Kwa furaha kubwa Amana Bank inahitimisha wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kusherehekea miaka 8 tangu kuanzishwa kwake. Sherehe hizi zimefanyika katika ofisi za makao makuu ya benki yaliyopo katika mtaa wa Ohio jengo la Golden Jubilee siku ya Ijumaa tarehe 22/11/2019 sambamba na matawi yake yote kwa nchi nzima.
Dira ya Amana Bank ni kuwa chaguo la kwanza na kiongozi katika utoaji huduma za kibenki zinazozingatia misingi ya kiislam. Dira hii inafuatiwa na dhamira ya kutoa huduma za kisasa na za kipekee kwa kuzingatia maadili kwa njia iliyo wazi kwa kupitia teknolojia za kisasa.
Akiongea katika hafla hiyo Mkurugenzi mtendaji Dr Muhsin Masoud alisema “Kauli mbiu ya wiki ya Huduma kwa wateja mwaka huu ilikua ni ‘Tabasamu lako, Furaha yetu’ ikiwa ni kiashiria katika uhamasishaji wa kiutendaji na ubunifu wa suluhu mbalimbali zinazopelekea kuwarahisishia wateja katika upataji wa huduma za kifedha ambazo zinakidhi mahitaji ya watanzania wa kipato cha kati na chini hususan wale wanye mahitaji ya mikopo midogo ya biashara, mikopo ya elimu na mikopo ya vikundi (Solidarity Group Financing) kwa lengo la kuwakomboa kiuchumi”.
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wake, Amana Bank inaendelea kuwaelimisha wazazi/walezi juu ya uwezeshwaji unaofanywa na katika masuala ya Elimu unaotolewa na Amana Bank wenye lengo la kupunguza mzigo wa ada za shule.
Amana Bank inaendelea kukua, na jitihada za kufikisha huduma zake maeneo mbalimbali ya Tanzania zinaendelea mwaka huu imefanikiwa kufungua tawi la tisa (9) Zanzibar na maandalizi ya kufungua tawi lake la 10 mkoani Dodoma mwaka 2020. Pia, ikiwa miongoni mwa benki chache nchini zenye mawakala zaidi ya 400 maeneo mbalimbali katika kurahisisha upatikanaji wa baadhi ya huduma zake.
Mkuu wa idara ya Masoko, Bw. Dassu Mussa, aliongeza na kusema kuwa “Sambamba na kauli mbiu ya “Tabasamu lako, Furaha yetu” Amana Bank, imeendeleza jitihada za kuongeza uwezo kwa wateja kuweza kupata huduma kiurahisi na kuwa miongoni mwa benki itakayo zindua mfumo wa kidigitali utakao fahamika kama Amana Bank MobileApp maalum kwa watumiaji wa simu janja; mfumo huu utazidi kuwarahishia wateja katika kupata huduma za kibenki kupitia simu zao na kwa gharama nafuu zaidi”
Uongozi na wafanyakazi wa Amana Bank kwa pamoja tunawashukuru sana wateja na wadau wa Amana Bank kutoka sehemu mbalimbali kwa kuwa pamoja nasi hadi leo na tunawakaribisha wote bila kujali dini au kabila katika matawi yetu kuendelea kupata huduma mbalimbali za kibenki.
Miaka 8 ya kuwahudumia katika njia Sahihi,
Tabasamu lako, Furaha yetu.