Search Open Account Branches Zakat Calculator Amana Bank Mtaani Facebook Instagram Linkedin

 

Amana Bank Kuwawezesha Wavuvi Visiwa Vya Unguja na Pemba

Posted on: Apr 13, 22 | News

Amana Bank kwa ushirikiano na USAID na ZAFICO tumefanikiwa kuwawezesha wavuvi mashine na boti zenye thamani ya shilingi milioni 108. Lengo letu ni kuwafikia wamiliki wa boti wenye uhitaji wa mashine za boti zaidi ya 800 na wavuvi 650 kwa visiwa vya Unguja na Pemba.

Tarehe 12/04/2022, Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr. Hussein Ali Mwinyi amewakabidhi mashine na boti 16 wavuvi wa Kijiji cha Shumba Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba.

“Kuendana na utekelezaji wa mipango ya uchumi wa buluu Amana Bank imetenga kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wa ngazi mbali mbali kwa ajili ya kukuza na kuendeleza biashara zao” Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank Abubakar Athman alisema wakati anatoa hotuba yake katika hafla fupi ya kukabidhi mashine na boti zilizo nunuliwa katika awamu ya kwanza.

x

Download Amana Bank App here →
appstore playstore