
Benki Kiganjani - Mobile Banking
Huduma ya Amana Mobile inakuwezesha kupata huduma mbalimbali za kibenki kwa kupitia simu yako ya kiganjani. Huduma hii inakuwezesha kupata huduma za kibenki wakati wowote, popote pale. Huduma ya Amana Mobile inakuwezesha kupata taarifa za akaunti yako, kufanya miamala mbalimbali, kulipia bili, kuhamisha fedha, kuomba kuwa na kitabu cha hundi na kununua muda wa maongezi ya simu. Ukiachilia mbali kuwa na huduma salama zaidi na yenye kukupa faragha, huduma hii pia ni muafaka sana na rahisi kuitumia. Waweza kuingia kwenye akaunti yako popote pale penye simu; iwe ni nyumbani, ofisini au hata kwenye gari lako.
HUDUMA ZITOLEWAZO NA AMANA MOBILE
- Kuulizia salio
- Taarifa fupi za akaunti
- Kununua muda wa maongezi wa simu
- Kulipia bili za huduma kama za DSTV, LUKU, STARTIMES, TTCL PREPAID/ BROADBAND/ UHURU ONE /SASATEL NA NECTA.
- Kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti moja kwenda nyingine ndani ya benki ya Amana.
- Mteja anaweza kupata taarifa ya akaunti yake
- Utajipatia kitabu cha hundi
- Kujulishwa kuhusu mabadiliko ya uuzwaji na ununuaji wa fedha za kigeni
SIFA NA FAIDA
- Rahisi kusajili na kutumia
- Ni huduma inayofuata kanuni za Kisharia
- Huduma za kibenki popote ulipo
- Pata huduma za kibenki saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki
- Rahisi kutumia
- Huduma za kibenki katika muda halisi
ANGALIA KIFURUSHI CHETU CHA KUANZIA!
"Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi."
(Surah Al Baqarah Aya 276)