
Uwezeshaji wa Nyumba
Hii ni huduma iliyoanzishwa kwa ajili ya kupunguza tatizo la mahitaji makubwa ya sehemu ya makazi na biashara nchini Tanzania uliosababishwa na kuongezeka kwa idadi ya watu, kupanuka kwa biashara na uchumi. Huduma hii inaendeshwa kwa mkataba wa Musharaka kupitia misingi ya kisharia ya kibenki. Utaratibu huu, kwa taratibu, utamwezesha mteja kumiliki nyumba yake.
SIFA
- Inaendeshwa kwa misingi ya Kisharia chini ya mkataba wa Musharaka
- Nyumba hiyo hiyo ndio itakuwa dhamana
- Muda wa makubaliano ni miaka 15
- Kiwango cha juu cha uwezeshwaji ni Tsh 100,000,000
- Mteja atachangia asilimia 20 ya gharama
- Umri wa mteja hadi wakati wa mwisho wa makubaliano ni miaka 60 na kushuka
- Bima ya eneo ni asilimia 1
- Gharama za uhamishaji zitabebwa na mteja
FAIDA
- Makubaliano yanayofuata misingi ya sharia
- Inamwezesha mteja kutimiza ndoto ya kuwa na nyumba
- Mtu maalum wa kumhudumia mteja
- Gharama nafuu
"Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watao zidishiwa.
(Surah Ar Rum, Aya 39)"