Kuweka Fedha

Wateja wa Amana Bank wanaotaka kuweka fedha katika akaunti zao sasa wanaweza kuweka fedha zao kwa wakala wa Amana Bank kwa kutumia simu zao za mkononi. Mteja kupitia simu yake, atachagua “kuweka fedha kwa wakala” na kufuata maelekezo.

Kutoa Fedha

Mteja ataingia katika mtandao wa simu na kwa kutumia namba yake ya siri atachagua “kutoa fedha kwa wakala” na kuingiza namba ya wakala. Baada ya hapo atafuata maelekezo mpaka mwisho. Hatimaye, mteja na mtunza fedha (cashier) watapata ujumbe mfupi wa maandishi wenye namba za kumbukumbu kuthibitisha kwamba fedha imehamishwa kwenye akaunti ya wakala kwa ajili ya kutolewa; baada ya hapo wakala atamkabidhi mteja fedha zake pamoja na risiti za muamala huo.

Amana Bank Mtaani:

Amana Bank Mtaani ni huduma mpya ya Amana Bank ambayo itatoa huduma ya kuweka na kutoa fedha kwa wateja wetu kupitia kwa mawakala wa benki. Mawakala na wateja wa huduma hii ya Amana Bank Mtaani watatumia huduma yetu ya simu ya mkononi. Technolojia hii itaunganisha simu au mashine ya manunuzi (Point Of Sale mashine) ya wakala wa benki na mitambo ya benki. Pamoja na huduma ya kuweka na kutoa fedha, mawakala wa benki pia wataweza kufungua akaunti za wateja wapya, kujaza fomu za ufunguzi wa akaunti, na kupokea taarifa mbalimbali zinazowezesha wateja kufungua akaunti katika matawi na makao makuu ya benki.

Kufungua Akaunti

Wateja wataweza kufungua akaunti za akiba kwa wakala wa Amana benki kwa kujaza fomu maalum ya kufungua akaunti kwa wakala na kuacha taarifa zake muhimu. Nyaraka zote muhimu zinazohitajika zitakusanywa na kunakiliwa na hatimae kupelekwa kwenye tawi la benki au Makao Makuu kwa ajili ya ufunguzi wa akaunti. Baada ya akaunti kufunguliwa, mteja atatumiwa ujumbe mfupi wa maandishi wenye namba ya akaunti yake, namba ya siri ya huduma ya benki kupitia simu ya mkononi, na pia atatakiwa kuweka fedha kwenye akaunti yake mpya.

Exchange Rates

19-Jun-2019 // TZS

CURRENCY
BUYING SELLING
UK Pound STG2,8172,966
Euro EUR 2,510 2,643
US Dollar USD 2,271 2,331
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"O believers, take not doubled and redoubled interest, and fear God so that you may prosper. Fear the fire which has been prepared for those who reject faith, and obey God and the Prophet so that you may receive mercy. (Surah Al ‘Imran, Verses 130-132)"