Amana Bank na Property International Katika Uwezeshaji wa ViwanjaAmana Bank Ltd na Property International Ltd (PIL) inayofuraha kubwa ya kutimiza miaka mitatu ya kufanya biashara pamoja kutimiza ndoto ya watanzania kwa kuwawezesha kumiliki viwanja katika maeneo salama yaliyopimwa na kupata hati miliki.


Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab amesema katika kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa kuwawezesha wateja zaidi ya 300 kumiliki viwanja vyao na kupatiwa hati halali.Aidha Bw.Rajab amesema kuwa, Katika mkopo huo watu wengi wameweza kunufaika kutumia viwanja hivyo kupata mkopo kupitia benki hiyo ili kuwezesha kuinua uchumi na kukuza biashara zao.

"Mteja anatakiwa atangulize asilimia 20 ya thamani ya kiwanja kama malipo ya awali na kulipa kiasi kilichobaki kwa muda uziodi mwaka mmoja na nusu ila kwa sasa tumeongeza hadi miaka mitatu,"amesema Rajab.

Amana Bank kutokana na kuwajali wateja tumeongeza muda wa malipo kutoka mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na kuwapunguzia faida toka asilimia 14 hadi asilimia 12 kwa mwaka mmoja.

Bw. Rajab ameeleza kuwa kuelekea Wiki ya huduma kwa wateja itakayoanza Novemba 19 mwaka huu, wateja watapata fursa ya kununua viwanja kwa punguzo maalum la bei na kutakuwa na mwakilishi kutoka PIL ndani ya wiki nzima ya huduma kwa wateja katika matawi yote Jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab amesema katika kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa kuwawezesha wateja zaidi ya 300 kumiliki viwanja vyao na kupatiwa hati halali.Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Property International (PIL), George Obado amesema kuwa wameweza kushirikiana na Benki ya Amana na kufanikisha watanzania wengi kupata viwanja vilivyopimwa pia wamekuwa wanafanya marekebisho ya barabara kwa kiwango cha Changarawe ili kufika kwenye maeneo yaliyo na viwanja.

Obado amesema, mbali na hilo kwa sasa viwanja vipo katika miradi ya Kimbiji Sea View Kigamboni, Magodani Mkuranga, Mapinduzi Residence, Chekeni Farm Mwasonga -Tundwi, Fukayose Residence Barabara ya Bagamoyo -Msata, The Dar es Salaam Automobile Zone (DAZ), Riverside Residence, Coco Palm, Royal Palm Mwasonga, African Palm Estate na Dege Residence.Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab(kushoto) akikata keki ya maadhimisho ya miaka mitatu na kampuni ya Property International Ltd (PIL) pamoja na Afisa mkuu Mwendeshaji wa Propert International Ltd(PIL) George Obado na baadhi ya wateja wa Viwanja.

Mkuu wa Idara ya Biashara Amana Bank Bw. Munir Rajab akikabidhi rasmi hati ya kiwanja kwa Bi. Aisha Sifana katika hafla ya kutimiza miaka mitatu ya kufanya biashara pamojaAmana Bank na Property International Limited.Bw. George Obado Afisa Muendeshaji Mkuu Property International Limited akikabidhi rasmi hati ya kiwanja kwa Bw. Stephano Mathias katika hafla ya kutimiza miaka mitatu ya kufanya biashara pamojaAmana Bank na Property International Limited.Picha ya pamoja ya uongozi na wafanyakazi wa Amana Bank na baadhi ya wateja waliofaidika na huduma ya Uwezeshaji wa viwanja wakionesha rasmi hati hizo.Picha ya pamoja wateja waliofaidika na huduma ya Uwezeshaji wa viwanja pamoja na maafisa wa huduma hiyo kutoka Amana Bank.Uongozi na wafanyakazi wa Amana Bank na Property International katika picha ya pamoja.Amana Bank na PIL kupitia bidhaa ya Plot Financing tutaendelea kushirikiana pamoja kuhakikisha watanzania wanapata makazi salama ya kuishi.

« Back to News & Media

Exchange Rates

22-Aug-2019 // TZS

CURRENCY
BUYING SELLING
UK Pound STG27212865
Euro EUR 2487 2,619
US Dollar USD 2,275 2,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"O, believers, fear Allah, and give up what is still due to you from the interest (usury) if you are true believers.
(Surah Al Baqarah Verse 278)"