Amana Bank na Uwezeshaji wa Madereva wa Taxify

Amana Bank na TY Services Limited ambayo ni kampuni inayoendesha mtandao wa Taxify hapa Tanzania zimesaini mkataba wa kuwawezesha madereva wa Taxify kumiliki vyombo vya moto (Motor vehicle Financing Scheme).

Lengo letu ni kuboresha usafiri na kuwaongezea madereva kipato kwa kuwawezesha kumiliki vyombo vya moto.


Meneja Kitengo Cha Biashara Amana Benki Bw. Dassu Mussa akifafanua jambo katika hafla hiyo kulia kwake ni Meneja wa Taxify Tanzania Bw. Remmy Eseke.


Uwezeshaji huu utafanyika katika vikundi, hivyo madereva watahitajika kuunda kikundi cha madereva kumi ambao watadhaminiana wenyewe.

Dereva ataweka amana isiyopungua 10% ya thamani ya chombo cha moto anachohitaji kuwezeshwa, amana hii itatumika kama dhamana mpaka dereva atakapomaliza kufanya marejesho.

Derava atatakiwa kuweka akiba ya TSH 15,000/= kila wiki ambayo itakuwa kama dhamana mpaka dereva atakapomaliza kufanya marejesho.

Dereva atafanya marejesho kulingana na makubaliano na benki katika kipindi kisichozidi miaka miwili.Meneja Kitengo Cha Biashara Amana Benki Bw. Dassu Mussa na Meneja wa Taxify Tanzania Bw. Remmy Eseke wakisaini makubalio.


Meneja Kitengo Cha Biashara Amana Benki Bw. Dassu Mussa na Meneja wa Taxify Tanzania Bw. Remmy Eseke wakisaini na kubadilishana makubaliano baina ya pande hizo mbili.


Benki itazingatia vigezo mbalimbali katika kutoa uwezeshaji huu ikiwemo dereva kuwa na uzoefu wa kutosha na rekodi nzuri.

Ni matarajio yetu maderava wa Taxfy watashangamkia fursa hii ili kuweza kumiliki vyombo vyao vya usafiri na kujiongezea kipato.


Meneja Kitengo Cha Biashara Amana Benki Bw. Dassu Mussa akiwasisitizia vijana kuchangamkia fursa hiyo adhim bila kukosa.« Back to News & Media

Exchange Rates

22-Aug-2019 // TZS

CURRENCY
BUYING SELLING
UK Pound STG27212865
Euro EUR 2487 2,619
US Dollar USD 2,275 2,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"O believers, take not doubled and redoubled interest, and fear God so that you may prosper. Fear the fire which has been prepared for those who reject faith, and obey God and the Prophet so that you may receive mercy. (Surah Al ‘Imran, Verses 130-132)"