Mnamo tarehe 19/11/2018 kwa furaha kubwa Amana Bank tumesherekea wiki yetu ya Huduma kwa Wateja ambayo kilele chake ilikua ni tarehe 24/11/2018, ambapo pia Amana Bank imetimiza miaka 7 toka ilipoanza kutoa huduma bora za kibenki mnamo tarehe 24/11/2011
Uongozi wa Amana Bank unawashukuru wateja, wadau wote na jamii kwa ujumla kwa kuwa nasi pamoja toka benki yetu ilipoanzishwa.
Tunawaomba wateja wetu na watanzania kwa ujumla watembelee matawi yetu kabla na baada ya wiki hii ya huduma kwa wateja ili waweze kupata huduma mbalimbali za kibenki, zawadi mbalimbali na fursa ya kuhudumiwa na Mkurugenzi mtendaji, Meneja Wakuu na wakuu wa idara mbalimbali.
Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Mwanza wakiwakatika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Dr.Muhsin Salim Masoud katika sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.
Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Lumumba katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.
Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Tandamti katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.
Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Tanga katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.
Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Arusha katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja punguzo maalumu litatolewa la bei za viwanja vinavyotolewa kwa njia ya mkopo na Amana Bank kwa kushirikiana na Property International limited itatolewa katika matawi ya Amana Bank Dar es Salaam
Sambamba na hayo wiki ya huduma kwa wateja imeambatana na uzinduzi rasmi wa mikopo ya vikundi ikiwa sehemu ya muendelezo wa benki yetu kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kujikwamua kiuchumi kama tunavyoendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kwa kuwapa mikopo inayoazia milioni moja hadi milioni kumi.
Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank kwa pamoja tunawashukuru sana wateja na wadau wa Amana Bank kutoka sehemu mbalimbali kwa kuwa pamoja nasi hadi leo na tunawakaribisha wote katika matawi yetu kuendeleakupata huduma mbalimbali kutoka Amana Bank.
Miaka Saba ya kukuhudumia katika njia Sahihi, Pamoja.