Search Open Account Branches Zakat Calculator Amana Bank Mtaani Facebook Instagram Linkedin Twitter

 

Hijja na Umrah sasa Imerahisishwa !!!

Posted on: Feb 06, 24 | News

Kwa kutambua umuhimu wa Hijja na Umra katika maisha ya Waislamu duniani kote, hivi karibuni Amana Bank ilifanya maboresho katika akaunti yake ya Hija na Umrah ambayo ilipelekea kuunda bidhaa kamili ya uwezeshwaji ambao utasimama katika kuondoa kikwazo kwa waislamu wa kulipia gharama za Hijja na Umra kwa mkupuo.

Katika hafla fupi iliofanyika kisiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Mufti Mkuu Zanzibar-Sheikh Saleh Omar Kabi, Katibu Mtendaji Umoja Taasisi za Hijja Zanzibar (UTAHIZA) - Shekh. Yusuf Salim na Katibu mtendaji kamisheni ya Wakfu na mali ya Amana- Shekh. Abdallah Talib. Mufti Mkuu Zanzibar Shekh Saleh amesisitiza kuwa huduma hii inaimarisha kwa kutimiza dhima hii kuu na kutoa suluhu kwenye maswala ya kifedha kwa jamii ya Kiislamu.

"Tunaelewa kwamba kukamilisha Hijja au Umra inahitaji juhudi kubwa za kujiwekea akiba ya fedha kidogokidogo mpaka kutimia. Lengo kuu la Amana Bank ni kufanya safari hii ya kiimani ipatikane kwa urahisi zaidi kwa wafanyakazi wote (wa serikali na taasisi binafsi) na wastaafu kutimiza ibada yao ya Hijja na Umrah kwa kuwapa suluhisho la uwezeshwaji unao kubalika na mfumo wa kifedha wa kiislamu (fiq muamalat)" alisema Abubakar Athman, Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank.

 

Amana Bank tumejitolea kutoa viwango vya faida vya ushindani ambavyo vinalingana na kanuni za fedha za Kiislamu, kuwapa wateja muundo wa bei wa haki na wa uwazi.
Tunatoa wito kwa wateja wote wenye nia ya kwenda kuhiji sasa au miaka ijayo bado hawajachelewa; Anza mahusiano yako nasi kwa kufungua akaunti yako ya Hajj& Umrah, Akaunti ya Mshahara, Akaunti ya Mstaafu au Akaunti ya Akiba Binafsi na uanze maandalizi ya safari yako adhim.

 

x

Download Amana Bank App here →
appstore playstore