SIFA

 • Ni akaunti inayofuata misingi ya sharia inayoratibiwa na Bodi ya usimamizi wa Sharia
 • Kiwango cha kufungulia akaunti ni Tsh 100,000 au Dola za Kimarekani 100
 • Kiwango cha chini kabisa cha kuendeshea akaunti ni Tsh 50,000 au Dola za Kimarekani 50
 • Inafuata mkataba wa Qardh ambapo mteja anaweza akalipwa kiasi cha fedha alichowekeza pale atakapohitaji
 • Utoaji wa fedha ni kwa kupitia hundi tu
 • Inapatikana kwa fedha za Kitanzania na Kimarekani

FAIDA

 • Uwezo wa kuweka na kutoa kiwango chochote cha fedha
 • Uwezo wa kutoa fedha saa 24, siku 7 za wiki kupitia mashine za ATM za Umoja Switch
 • Utulivu wa nafsi kwani mteja amehifadhi hela zake kwenye benki yenye kufanya shughuli za kihalali
 • Utapatiwa taarifa za akaunti yako bure kila mwezi
 • Utanufaika na huduma ya benki kulipa fedha kwenye akaunti nyingine kwa kiwango mlichokubaliana kila mwezi
 • Utapewa haraka kitabu cha hundi
 • Utapewa haraka kadi ya ATM
 • Usajili mwepesi wa huduma za kibenki kupitia mtandao na ujumbe mfupi
 • Hakuna gharama zilizojificha

VIFAA VYA AKAUNTI

 • Kadi ya ATM ya Umoja Switch
 • Kitabu cha hundi chenye kurasa 50 au 100
 • Huduma ya kibenki kupitia Ujumbe mfupi na mtandao

MAHITAJI YA KUFUNGULIA AKAUNTI:

 • Fomu ya kufungua akaunti kwenye Benki ya Amana iliyojazwa
 • Picha moja ya saizi ya pasipoti
 • Nakala ya leseni mpya ya udereva / kitambulisho cha mpiga kura/ hati ya kusafiria au kitambulisho cha taifa
 • Barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa au mwajiri wako au wakili wako au mteja wa benki ya Amana au risiti za malipo ya huduma za maji, umeme au simu
 • Hati ya kuishi ama kufanya kazi nchini
 • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.
(Surah Al Baqarah Aya 278)"