Nani mwenye sifa za kuomba uwezeshaji katika benki ya Amana?

Watu binafsi/ makampuni yaliyosajiliwa katika biashara za halali na yanakidhi kanuni zetu na pia yanakubali mashariti yetu ya uwezeshaji.

Ni nyaraka zipi zinazohitajika kwa mteja ili aombe mkopo?

Nyaraka zitakiwazo hutofautiana kulingana na aina ya biashara. Tunakushauri uwaulize wafanyakazi wa benki au soma vipeperushi vyetu.

Je muda wa marejesho huwa hadi miaka mingapi?

Mpaka miaka mitatu

Hivi benki ya Amana inatoa uwezeshaji wa nyumba?

Ndio tunawawezesha wateja wetu katika kununua vifaa vya ujenzi kwa kuwataka walipe ndani ya miaka mitatu. Mbali na hivyo, benki ina mpango pia wa kutoa uwezaji huu kwa njia ya ushirika kwa marejesho ya kipindi kirefu.

Wakati gani mnagawa faida kwa wateja wenu?

Kwa wateja wa akaunti za akiba, faida inalipwa mara nne kwa mwaka, mwisho wa miezi ya machi, juni, septemba na disemba. Kwa wateja wa akaunti maalum, faida inalipwa mwishoni mwa muda tuliokubaliana.

Je benki hii inaweza kulipa mkopo wa mteja wake mwenye deni benki nyingine?

Benki hii inaweza kulipa mikopo hiyo kupitia mkataba wa Qardh au Tawarruq inapoona kuna haja ya kufanya hivyo.

Kwa nini mchakato wa uwezeshaji wa benki hii unachukua muda mrefu kuliko benki za riba?

Si kweli, ahadi yetu ni kutimiza maombi ya kuwezeshwa kibiashara ndani ya siku 5.Tunawaomba wateja wetu wawasilishe taarifa zote zinazohitajika kwa wakati ili kupunguza muda wa kuchanganua maombi yako. Kwa bahati mbaya, wakati mwingine wateja huwa hawakamilishi taarifa zao kwa wakati na kupelekea kuchelewa kukidhiwa haja yao kwa wakati.

Je benki inatoa mikopo ya nyumba?

Bado hatujaanza, lakini mikopo ya nyumba ipo katika mipango ya benki.

Tunawekaje viwango vyetu vya faida katika Murabaha au mikopo?

Katika Murabaha(kununua na kuuza kwa faida), viwango vya faida tunayoweka katika muamala vinatemeana na gharama ya fedha katika soko na hatari zilizomo katika muamala. Iwapo hatari ni kubwa na faida nayo inapanda, hili ndo jambo la msingi katika kupanga faida yetu.

Tunawekaje viwango vya faida kwa ajili ya wateja wetu?

Faida inayogawiwa kwa watunza fedha Amana Bank inategemeana na faida itakayopatikana kutokana na shughuli za biashara za benki katika kipindi fulani na kwa kuzingatia viwango vilivyopo katika soko.

Kwa nini benki ya Amana inahitaji dhamana?

Mikopo ina hatari kubwa inayohitaji ulinzi na usimamizi sahihi ili kuepuka hasara inayoweza kujitokeza kwa kupotea fedha za wamiliki na wateja wengine walioweka fedha kwetu iwapo aliyekopa atashindwa kulipa marejesho yake ipasavyo. Ili kuzuia jambo hili lisitokee, benki za biashara zinatakiwa na sheria za nchi kuwa na dhamana ya kutosha kama njia moja wapo itakayosaidi benki kurejesha fedha zake.

  • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watao zidishiwa.
(Surah Ar Rum, Aya 39)"