Uongozi wa benki:

Bodi yetu ya wakurugenzi inaundwa na wafanyabiashara wakubwa pamoja na wasomi wenye uzoefu tofauti tofauti ambao wanasaidia kuipa benki muongozo. Benki ina bodi za kamati mbalimbali ambazo zinasaidia bodi kuu. Ikiwa kama mwanzilishi wa benki zenye kufuata misingi ya sharia, bodi ya usimamizi wa sharia ndio chombo kinachothibitisha bidhaa, huduma na michakato ya benki yetu. Bodi ya usimamizi wa sharia inaundwa na wanazuoni wa Kiislamu kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Wafanyakazi wetu:

Benki ya Amana ni mwajiri mwenye kutoa haki sawa kwa wote na imeajiri wafanyakazi waliojitolea kazini, wenye weledi na uzoefu wa miaka mingi. Wafanyakazi hawa wamepata mafunzo ya hali ya juu na wana uwezo wa kutoa huduma bora kabisa kwa wateja wetu. Benki ya Amana ina huduma za kibenki zenye kukidhi mahitaji ya wateja wake Waislamu na hata wale wa dini nyingine. Haijalishi kama ni mtu mmoja ama ni shirika, tunaweza tukakupa huduma za kibenki za hali ya juu.

Maana ya Amana:

Kwa lugha ya Kiswahili, Amana inamaanisha uaminifu. Nembo yetu inawakilisha usalama na mafanikio / ustawi, kwa maana kwamba ukiwa na Benki ya Amana upo katika mikono salama. Nembo yetu inawakilisha usalama, haki, tatuzi za kifedha zilizojikita kwenye maadili, uwezeshwaji wa kifedha kwa wadau wetu, ushirikishwaji, majukumu ya kijamii na ufanyaji kazi wa hali ya juu.

Kiongozi katika huduma za kifedha:

Moja ya sababu iliyopelekea kuanzishwa kwa benki ya Amana ni uhitaji wa kuwepo kwa mbadala wa huduma za kawaida za kibenki, na hivyo kuleta mfumo wa kibenki wenye maadili na usawa. Kama mwanzilishi, Benki ya Amana inatambua jukumu kubwa iliyokuwa nayo ya kuhakikisha inaendelea kuwa mfano kwenye ukuaji wa mifumo ya kibenki kwa misingi ya Kiislamu huku ikichangiwa na teknolojia za kisasa. Benki ya Amana ina lengo la kupanua wigo wake, sehemu mbalimbali Tanzania na hapo baadae, hata nje ya mipaka yake ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma zake kwa urahisi kwa kupitia njia mbalimbali za utolewaji wa huduma.

  • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. Na uogopeni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa.. (Surah Al ‘Imran, Aya 130-132)"