Amana Bank Wiki ya Huduma kwa Wateja - 2018

Mnamo tarehe 19/11/2018 kwa furaha kubwa Amana Bank tumesherekea wiki yetu ya Huduma kwa Wateja ambayo kilele chake ilikua ni tarehe 24/11/2018, ambapo pia Amana Bank imetimiza miaka 7 toka ilipoanza kutoa huduma bora za kibenki mnamo tarehe 24/11/2011

Uongozi wa Amana Bank unawashukuru wateja, wadau wote na jamii kwa ujumla kwa kuwa nasi pamoja toka benki yetu ilipoanzishwa.

Tunawaomba wateja wetu na watanzania kwa ujumla watembelee matawi yetu kabla na baada ya wiki hii ya huduma kwa wateja ili waweze kupata huduma mbalimbali za kibenki, zawadi mbalimbali na fursa ya kuhudumiwa na Mkurugenzi mtendaji, Meneja Wakuu na wakuu wa idara mbalimbali.


Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Mwanza wakiwakatika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Dr.Muhsin Salim Masoud katika sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Lumumba katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.


Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Tandamti katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.


Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Tanga katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.Uongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Arusha katika picha ya pamoja sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.


Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja punguzo maalumu litatolewa la bei za viwanja vinavyotolewa kwa njia ya mkopo na Amana Bank kwa kushirikiana na Property International limited itatolewa katika matawi ya Amana Bank Dar es Salaam

Sambamba na hayo wiki ya huduma kwa wateja imeambatana na uzinduzi rasmi wa mikopo ya vikundi ikiwa sehemu ya muendelezo wa benki yetu kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kujikwamua kiuchumi kama tunavyoendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kwa kuwapa mikopo inayoazia milioni moja hadi milioni kumiWafanyakazi wa Amana Bank Tawi la Nyerere wakiwakatika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Dr.Muhsin Salim Masoud katika sherehe za Wiki ya huduma Kwa Wateja.


Mkurugenzi Mtendaji Dr.Muhsin Salim Masoud akitoa ufafanuzi na maelekezo kwamteja katika sherehe za Wiki ya huduma Kwa WatejaMkurugenzi Mtendaji Amana Bank Dr. Muhsin Salim Masoud akiwa dawati la huduma kwa watejakwa makini kabisa akimsikiliza mteja kutoka Tawi la Amana Bank Mwanza.


Meneja kitengo cha biashara Amana Bank Bw. Dassu Mussa akitoa huduma kwa wateja katikadawati la mapokezi Amana Bank Tawi la Nyerere.Mkuu wa Idara ya biashara Bw. Munir Rajab akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wateja wa Amana Bank tawi la Arusha.Aidha katika kuwajali wateja wetu,pia tumezindua rasmi kampeni maalumu ya NUFAIKA NA AKIBA YAKO.Katika kampeni hii,wateja wetu watakao weka akiba isiopungua milioni tano kwa mwezi kwa muda wa miezi mitatu mfululizo watapata nafasi ya kushinda pikipiki aina ya TVS.Picha ya pamoja: Mkurugenzi Mtendaji Dr.Muhsin Salim Masoud na Meneja wa Tawi la Mwanza Bw.Athuman Julius na wateja wa Amana Bank tawi la Mwanza katika sherehe za Wiki ya huduma Kwa WatejaUongozi na Wafanyakazi wa Amana Bank kwa pamoja tunawashukuru sana wateja na wadau wa Amana Bank kutoka sehemu mbalimbali kwa kuwa pamoja nasi hadi leo na tunawakaribisha wote katika matawi yetu kuendeleakupata huduma mbalimbali kutoka Amana Bank.


Miaka Saba ya kukuhudumia katika njia Sahihi,


Pamoja.

« Habari na Matukio
  • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua.
(Surah Al Baqarah Verse 280)"