Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa-SABA SABA 2019

Kwa namna ya pekee zaidi na awamu ya 4 mfululizo Amana Bank imeshiriki Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam maarufu kama SabaSaba. Katika kutekeleza sera ya upatikanaji wa Elimu bora kwa watoto ambao ni taifa la kesho na kujali watu hususani wazazi au walezi,Amana Bank ilipata fursa ya kunadi na kuonesha bidhaa ya kipekee iitwayo Elimu Financing yaani uwezeshaji katika Elimu.

Elimu Financing au Uwezeshaji katika Elimu ni bidhaa ya kipekee na ya kwanza kubuniwa na Amana Bank yenye dhumuni la kuwezesha wazazi au walezi katika kurahisisha ulipaji wa mahitaji ya shule ya watoto/wanafunzi. Mahitaji hayo ni kama vile Ada,Malazi,Nyenzo za kujifunzia shuleni n.k.


Mfanyakazi wa Amana Bank akitoa ufafanuzi wa huduma za Amana Bank kwa wateja waliotembelea banda la Amana Bank katika viwanja vya Sabasaba


Katika Maonesho ya Kibiashara ya 43, Amana Bank ilijikita rasmi katika kutoa elimu ya huduma hii na njia mbalimbali za kuwezesha wazazi/walezi katika kupata huduma ya Elimu Financing sambasamba na uwezeshaji wa aina nyingine ikiwemo wa mali,bisahara n.kLakini pia katika maonesho haya kwa kipekee zaidi huduma za aina mbalimbali ziliweza kutolewa papo hapo kwa watu wa aina zote ikiwemo:Kufungua Akaunti za akiba za aina mbalimbali pamoja na ubadilishaji wa fedha za kigeni papo hapo.Kama ilivoada ya siku ya maadhimisho haya yaani tarehe 7/7/2019 uongozi na wafanyakai wa Amana Bank kwa pamoja wote walikuwepo katika viwanja hivo kuhakikisha watu wote wanaofika katika banda la Amana Bank wanapata huduma ya kipekee sambamba na kuuliza maswali mbalimbali ya mfumo wa kibenki unaozingatia misngi ya kiisalmu pamoja na kujipatia zawadi kem kem kutoka Amana Bank.
Baadhi ya wateja mbalimbali waliozawadiwa zawadi kem kem katika banda la Amana Bank viwanja vya Sabasaba


Aidha katika kuimarisha mahusiano na kutambua uwepo wa washiriki wengine katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba, menejimenti na wafanyakazi wa Amana Bank kwa pamoja pia walipata fursa ya kutembelea katika baadhi ya mabanda ya wafanyabiashara hasa wajasiriamali na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali na kupata fursa ya kufahamu utendaji,changamoto moto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kufanikisha biashara zao lakini pia kujua jinsi gani kama taasisi ya kifedha inaweza kuwawezesha ili kuimarisha taifa letu la wachapakazi. Miongoni mwa mabanda waliotembelea ni Vodacom,Small Indurstries Development and Organisation (SIDO),Asas Diaries Limited , Azam na Property International Limited (PIL).


Viongozi na wafanyakazi wa Amana Bank katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Propert International Limited (PIL) ,ndani ya viwanja vya Sabasaba.


Wafanyakazi wa Amana Bank wakiongozwa na Meneja Mkuu Uthibiti na Usaidiz Muhidin Ally katika picha wakipata ufafanuzi wa huduma ya MPESA-kutoka kwa Afisa Masoko wa Vodacom katika viwanja vya Sabasaba.


Meneja Mkuu Uthibiti na Usaidiz Muhidin Ally kutoka Amana Bank katika picha akipokea bidhaa ya Asas kutoka kwa Afisa Masoko wa Asas Diaries Limited katika viwanja vya Sabasaba.


Viongozi na wafanyakazi wa Amana Bank katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SIDO ndani ya viwanja vya Sabasaba


Amana Bank tunazidi kubuni bidhaa zinazoweza kuwafikia watu wa mbalimbali kulingana na mahitaji yao. Lakini pia tunatoa shukran za dhati kwa waandalizi wa maonyesho hayo na wageni wote walioweza kufika katika banda letu na pia tunawakaribisha watanzania wote kufika katika matawi yetu kujiunga nasi ili waweze kufurahia huduma bora za kibenki zinazofata misingi ya kiislamu Tanzania.

« Habari na Matukio
  • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.
(Surah Al Baqarah Aya 278)"