Kwa nini benki yenu ina matawi mengi Dar es Salaam?

Dar es Salaam ndio mkoa wenye shughuli nyingi za kibiashara na idadi kubwa ya watu kuliko mkoa mwingine wowote hapa nchini.Idadi kubwa ya watu na na uwingi wa biashara katika mkoa huu, inaisukuma benki kuanzisha matawi mengi ili kukidhi lengo la soko kiufanisi zaidi. Hata hivyo, tumefungua matawi yetu mengine matatu katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Tanga na pia tunatarajia kufungua matawi mengine zaidi katika mikoa mengine

Je Amana bank imesalimika na kutoa / kupokea riba kwa kuweka na kutoa fedha zake katika akaunti za benki kuu ya Tanzania(BOT)?

Benki ya Amana inaendesha shughuli zake na benki kuu ya Tanzania bila ya kutoa wala kupokea riba. Sheria ya kifedha, zinatutaka kutunza katika akaunti ya benki kuu asilimia 10 ya akiba(deposit) zetu. Pia ili kuwezesha malipo ya cheki inatutaka kuwa na fedha katika akaunti yetu. Katika akaunti hizi zote hatutoi wala kupokea riba.

Je benki ya Amana inamilikiwa na wawekezaji kutoka nje ya nchi?

Hapana, sehemu kubwa ya wawekezaji wa benki hii ni wafanyabiashara maarufu wa Tanzania. Pamoja na hivyo, baaadhi ya hisa zinamilikiwa na wageni.

Kwa nini ni rahisi kwa msikiti kufungua akaunti katika benki ya riba kuliko benki ya amana?

Hapana ugumu wowote, isipokuwa kinachohitajika ni kuusajili msikiti na kukamilisha vigezo vyote vinavyohitajika. Akaunti za misikiti zinapata zinafunguliwa akaunti ya kipekee iitwayo Ihsaan.

Kwa nini benki ya Amana haitoi aina nyingine za uwezeshaji zaidi ya hii ya murabaha?

Mkataba wa murabaha una manufaa yake na mipaka yake. Miongoni mwa manufaa yake; ni mkataba rahisi kufahamika na kutekelezeka kutokana na uchache wa hatari(risk) zake. Zaidi ya hayo, benki ya Amana kwa kutambua mipaka ya utaratibu huu inatumia mkataba wa Qardh na pia ina mpango wa kutumia aina nyingine za mikataba kadri sheria za kibenki zinakavyoruhusu.

Je mnapokea dhamana zilizo nje ya mkoa wa Dar - es - Salaam wakati wa kuomba mkopo?

Dhamana zilizo nje ya Daressalaam zinakubalika ikiwa tu zina thamani ya kutosha ya kuudhamini mkopo.

Kazi kubwa ya benki ya kiislam ni kusaidia kunyanyua hali za kimaisha za watu. Je benki ya Amana ina mpango wa kuwasaidia watu wenye kipato cha chini?

Kazi kubwa ya benki ya kiislam ni kusaidia kunyanyua hali za kimaisha za watu. Je benki ya Amana ina mpango wa kuwasaidia watu wenye kipato cha chini?

Kwa nini benki ya Amana inawahudumia wasio waislam?

Benki ya Amana ni kwa ajili ya watu wa imani zote bila ya ubaguzi wowote na hakuna vikwazo vyovyote katika sharia inayozuia kuwahudumia wasio waislamu. Benki ya Amana inatambua fika kwamba huduma za kifedha ni sehemu ya mahitaji ya lazima ya mwanadamu na malengo ya sharia, kanuni na taratibu, ni kuleta manufaa na kukidhi mahitaji ya lazima ya mwanadamu.

Ni nani wanahisa(wamiliki) wa benki hii?

Wanahisa(wamiliki) wa benki hii ni makampuni na watu binafsi. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tazama majina yao katika urari wa ripoti za fedha ulio katika website yetu: www.amananbank.co.tz

  • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.
(Surah Al Baqarah Aya 278)"