Kwa nini benki ya Amana haifungi shughuli zake wakati wa sala ya Ijumaa?

Kuendelea na shughuli za kibiashara kipindi cha swala ya ijumaa ni jambo lisiloruhusiwa kwa mukallaf(muislam mwanaume, baleghe,mkazi wa mji na mwenye akili timamu) lakini inaruhusiwa kwa wengine. Bodi ya sharia ya benki ya Amana imepitisha uamuzi wake juu ya benki hii kuendelea na biashara wakati wa swala ya ijumaa ili mradi tu watakaokuwa wanatoa huduma hiyo si wale wanaolazimika kutekeleza ibada hii(wanawake au wasio waislam). kwa wale wanaolazimika na kuruhusiwa kwenda kutekeleza ibada hii kisha wakaamua kwa utashi wao kutoenda, kosa ni lao si la benki, kwani benki tayari imeshawapa ruhusa ya kwenda kutekeleza ibada hii.

Baadhi ya huduma ambazo benki ya Amana inatoa zinaingia katika hali ya kukosa uhakika (gharar) ambayo inaenda kinyume cha kanuni za sharia. Kwa mfano Dhamana za kibenki (Guarantee),je ni kweli jambo hili?

Benki ya Amana inatoa aina mbalimbali za dhamana za kibenki (guarantee) kupitia mkataba wa kafala(udhamini) ambao unaruhusiwa kisharia. Dhamana hizi huusisha sehemu ndogo sana ya kutojulikana kwa matokeo, hali ya kuwa hali hiyo haliepukiki maana ni vigumu kujua 100%. Sharia inakataza gharar kubwa ambayo inaweza kuepukika.

Thamani ya pesa hushuka katika kipindi cha mfumuko wa bei ili kuwafidia wakopeshaji kwa kupungua thamani ya mtaji wao utaratibu wa kulinganisha thamani ya pesa zao wakati wanapokopesha na uwezo wake wa kununua vitu katika wakati fulani imeshauriwa kufuuatwa.. Je utaratibu huu unakubalika katika mtazamo wa kiislam?

Haukubaliki. Mtazamo wa Uislamu ni kuwa kwanza mfumuko wa bei ni tatizo ambalo serikali yoyote lazima ihakikishe unadhibitiwa ipasavyo ili uchumi wa nchi uiimarike. Pili, kitendo cha kukopesha ni cha kheri na chenye malipo mara kumi ya sadaqa. Hivyo, ingawa thamani yapotea lakini wema huu malipo yake ni makubwa na hayashuki thamani yake. Na hii ndio nia impasayo mtu kuwa nayo anapokopesha ili amsaaidie mwenzie. Kwa kutambua tatizo la mfumuko wa bei kuwa linaathari mbaya katika mfumo wa fedha, benki za kiislamu zinaweza kutumia mikataba ya Ushirika ambayo matokeo na tija inayopatikana huzingatia moja kwa moja mfumuko wa bei unapotokea.

Kwa nini benki ya Amana haigawani hasara na wateja wake?

Kanuni za kifedha za nchi zilizopo hivi sasa hazitambui utaratibu wa kugawana faida na hasara. Kwa hiyo, fedha za wateja zinalindwa zisibebe hasara itakayosababishwa na mazingira ya kibiashara ya benki. Hata hivyo, ingawa kugawana faida na hasara ndio msingi wa mkataba wa Ushirika,utaratibu huu una changamoto zake kiutendaji hususan katika soko ambalo benki za riba ziko imara katika nchi kama Tanzania. Hadi hapo mkanuni zitakapobadilika benki ya Amana inalazimika kubeba hasara zote na kugawana faida tu na wateja wake.

Benki ya Amana inamchukulia hatua gani mteja anaechelewesha marejesho yake?

Endapo mteja anakabiliwa na matatizo yanayomsababisha kuchelewesha marejesho kwa muda husika, atalazimika kuitarifu benki juu ya hilo na kueleza sababu za msingi za kuchelewa kwake pamoja na kuomba kuongezewa muda wa marejesho. Benki itatathmini sababu alizozitoa na endapo itaridhika, itamuongezea muda baada ya kumshauri mteja. Lakini, endapo mteja hakuitaarifu benki, benki itamzingatia kuwa ni amepuuza wajibu wake na itamlazimisha kulipa. Wateja watalazimika kulipa kiasi fulani cha fedha kama sadaka pale wanapopuuza kulipa kwa wakati marejesho yao bila taarifa au sababu ya msingi.

Benki ya Amana inatumia mikataba gani kwa sasa?

Mikataba inayotumika kwa sasa ni mudharaba(mteja anaweka fedha na benki inawekeza), Murabaha(Kununua na kuuza kwa faida), Qardh( kukopesha bila faida), Kafala(udhamini) na ijaratul A’mal.

Je inakubalika kisharia katika mkataba wa udhamini (Guarantee) kumtoza mteja kiasi kinacholingana na kile kinachotozwa na benki za riba??

Benki za kiislam duniani kote zinaweka tozo katika huduma ya udhamini inayoitoa. Benki hizi zinaweka tozo hili kwa sababu zinabeba gharama za usimamizi wa huduma hii pamoja na kujiingiza katika hatari za kifedha endapo benki italazimika kutoa fedha. Tofauti kubwa kati ya udhamini wa benki ya Amana na ule wa benki za riba ni pale tu benki inapotakiwa kulipa, benki za riba zinaugeuza udhamini huu kuwa ni mkopo wa riba wakati ambapo benki za kiislam zinauhesabu malipo iliyolipa ni mkopo ambao unalipwa bila tozo za ziada.

Je inakubalika kisharia kumtoza mteja anayeendesha akaunti yake chini ya kiwango cha chini cha kuendesha akaunti, kwa sababu ya kushindwa kuweka fedha siku anayofungua akaunti yake?

Sio sahihi kutoza tozo aina hii kwa mteja ambaye hajawahi kuweka fedha kabisa katika akaunti yake. Mameneja wa matawi wanalazimika kurejesha maramoja tozo hii kwa wateja ikithibitika wametozwa. Tokea mwezi mei 2013 benki imepiga marufuku na kuondoa kabisa tozo hii katika akaunti zote za akiba

Kwa nini tumekiingiza kifungu cha adhabu kwa mteja anapochelewa kulipa marejesho ilhali baadhi ya wanazuoni wameharamisha kitendo hiki?

Bodi yetu ya usimamizi wa Sharia imeeleza kwamba kifungu hiki hakibatilishi mkataba wa Murabaha kwa kuwa lengo lake ni kuwavunja moyo wale wenye malengo ya kukopa bila kuwa tayari kulipa kikamilifu kitendo kinachosababisha hasara kwa benki. Ndani ya kifungu hiki, mteja anajifunga mwenyewe juu ya kutekeleza wajibu wake na pia kuitia imani benki kuwa ipo tayari kulipa kwa wakati. Zaidi ya hivyo, tozo hii inapelekwa moja kwa moja katika mfuko wa sadaka. Jambo la kuzingatiwa hapa ni kwamba benki haifadiki na chochote kutoka katika tozo hii, isipokuwa inazigawa fedha hizo kwa watu wanaostahiki chini ya usimamizi wa bodi yetu wa wataalamu wa Sharia. Jambo hili pia limeridhiwa na bodi ya Sharia ya taasisi ya AAOIFI, iliyopo Bahrain.

Kwa nini tunakata bima za riba wakati hazikubaliki kisharia?

Wateja wa benki na umma kwa ujumla wana maslahi katika benki kwa kuwa wameipa amana yao ili iendeshe biashara. Biashara kubwa ya benki ni uwezeshaji kupitia mikataba tofautitofauti na hivyo basi huitaji dhamana. Dhamana kwa kawaida hukabiliwa na hatari nyingi kama vile moto na hatari nyinginezo ambazo zaweza kuishusha thamani yake dhidi ya deni lake. Kwa kulinda maslahi ya umma na mfumo wa kifedha wa nchi na kwa kuwa hatuna bima ya kiislam, tunalazimika kutumia bima za riba mpaka tutakapopata bima ya kiislam(takaful). Hii ni dharura inayokubalika kwa sababu kama tutashindwa kuwa na bima umma utapata hasara kubwa ambayo itapelekea kuanguka kwa mfumo wa fedha

Je naweza kujua kisio la faida ninayoweza kuipata kutoka katika fedha ninayowekeza?

Ndio. Benki ina taarifa juu ya kiasi gani kililipwa siku za nyuma ambayo inaweza kukupa makadirio ya kile unachoweza kupata au itakupa kiwango ashiria (indicative rate) cha faida kulingana na uwekezaji uliofanya. Hata hivyo, tutalipa faida halisi iliyopatikana kutoka katika uwekezaji ndani ya kipindi husika na si lazima kiwafikiane na kiwango ashiria.

Katika mkataba wa murabaha, ni nani anayelipia kugharamia tozo za kutoa mzigo bandarini?

Ndio. Benki ina taarifa juu ya kiasi gani kililipwa siku za nyuma ambayo inaweza kukupa makadirio ya kile unachoweza kupata au itakupa kiwango ashiria (indicative rate) cha faida kulingana na uwekezaji uliofanya. Hata hivyo, tutalipa faida halisi iliyopatikana kutoka katika uwekezaji ndani ya kipindi husika na si lazima kiwafikiane na kiwango ashiria.

Endapo tatizo kubwa litamtokea mteja, je anaweza kutoa fedha kutoka katika akaunti yake ya hijja?

Ndio, anaweza kuiomba benki kutoa fedha yake kutoka katika akaunti hii.

Ni huduma gani tofauti inazozitoa akaunti ya wanawake?

Kuhudumiwa kipekee na watunza fedha wanawake. Pia kupata nafasi ya bure ya mualiko kushiriki kongamano la mwaka la wanawake linalodhaminiwa na benki.

Kwa nini benki ya Amana haitoi mikopo midogomidogo kama zinavyofanya benki nyingine?

Benki ya Amana inahisi kwamba kwa mteja kuanza kufaidika ukilinganisha na gharama za lazima katika kupata mikopo, ni lazima aanze na kiasi kisichopungua milioni 25. Hata hivyo, tunatambua kwamba baadhi ya wateja wetu wana mahitaji ya chini ya kiasi hiki. Hivyo basi, benki inakiri kuwepo kwa upungufu huu na itajitahidi kutafuta njia nzuri za kuwawezesha wateja wetu mbalimbali kupata mkopo.

  • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua.
(Surah Al Baqarah Verse 280)"