Dr. Muhsin Salim Masoud-Mkurugenzi Mtendaji

Kabla ya kuanza kazi kama Mkuregenzi Mtendaji wa Amana Benki (Mei, 2015) Dkt. Muhsin alikuwa ni muhadhiri na mkuu mshiriki wa shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Dkt. Muhsin pia aliishaitumikia bodi ya benki ya Amana na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Ukaguzi, Tahadhari na Uadilifu wa kibiashara, tangu kuanzishwa kwa benki hii (Novemba, 2011).


Ana shahada ya uzamivu ya masuala ya utawala wa biashara kutoka kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam aliyotunukiwa mwaka 2007. Shahada yake ya uzamivu ilihusu Usimamizi wa wadau na wajibu wa mashirka kunyanyua jamii zao. Kabla ya kupata shahada yake ya uzamivu, alipata shahada ya kwanza ya biashara iliyojikita kwenye uhasibu kwenye kitivo cha Uongozi cha Chuo cha kiislamu cha Uganda. Ana shahada ya uzamili ya fedha kutoka chuo cha Strathclyde kilichopo Uingereza na ya uana Falsafa kutoka chuo kikuu cha Umea kilichopo nchini Sweden.


Dkt. Muhsin ana uzoefu wa kufundisha masuala ya kibiashara. Kama mwanazuoni wa chuo cha biashara cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Muhsin ameshiriki kwenye tafiti na kozi za muda mfupi. Sehemu kubwa ya tafiti zake zilikuwa ni kwenye masuala ya biashara na jamii, maadili ya kibiashara, elimu ya uhasibu na masuala mengine ya wadau wa biashara. Amesimamia wanafunzi mbalimbali wanaochukua masomo ya uzamili na uzamivu. Na pia ametoa machapisho kwenye majarida ya ndani na nje ya nchi kwenye masuala ya menejimenti ya biashara na uhasibu na pia ameandika kwenye machapisho ya makongamano kadhaa ya kimataifa.


Kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam mwaka 1999, Dkt. Muhsin alifanya kazi kama muhadhiri kwenye Chuo cha Kiislamu cha Uganda ambapo ni mahali alipoanza kazi yake ya ukufunzi mnamo mwaka 1995. Zaidi ya hayo, Dkt. Muhsin pia ni mmoja wa wajumbe wa seneti ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.

Mr. Muhidin Ally - Support and Control

Mr. Saidi Mbaruku - Finance

Mr. Dassu Mussa - Commercial

Mr. Ayoub Korogoto - Legal and Company Secretary

Mr. Muhsin Mohamed - Sharia and Product

  • Mastercard

Viwango vya Kubadili Fedha

22-Aug-2019 // TZS

FEDHA
KUNUNUA KUUZA
UK Pound STG 2,721 2,865
Euro EUR 2,487 2,619
Us DollarUSD
2,2752,315
Full Rate Sheet

Customer Service:

Tel. 0657 980000

Email: customerservice@amanabank.co.tz

"Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. Na uogopeni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa.. (Surah Al ‘Imran, Aya 130-132)"